Michezo

Nico Rosberg ashinda mbio za Singapore Grand Prix

Nico Rosberg, dereva wa Mercedes, amefanikiwa kuwa wa kwanza katika kufuzu Singapore Grand Prix, ameshinda mbio hizo ambazo ni mbio zake za 200 katika Formular 1.

3887198b00000578-3795231-image-a-29_1474208654769

Mercedes driver Nico Rosberg of Germany celebrates after winning the Singapore Formula One Grand Prix on the Marina Bay City Circuit Singapore, Sunday, Sept. 18, 2016. (AP Photo/Yong Teck Lim)

Rosberg ambaye hii ni mara yake ya kwanza kushinda Singapore Grand Prix ,huu ni ushindi wake wa 3 mfululizo na wa 8 katika msimu huu wa Formular 1.

388745dc00000578-3795231-image-a-55_1474209651309

Daniel Ricciardo wa Redbull amekamata namba 2 huku bingwa mtetezi Lewis Hamilton ambaye alipata tatizo la breki katika gari lake amekamata nafasi ya 3.

Bingwa wa Singapore Grand Prix mwaka jana Sebastian Vettel wa Ferrari ambaye leo alianza wa mwisho kufuatia kupigwa penati lakini akamaliza mbio akiwa namba 5.

Ushindi wa Rosberg leo umemfanya apae kileleni katika msimamo wa madereva msimu huu akiwa na pointi 273 na Hamilton sasa yupo namba 2 akiwa na pointi 8 nyuma ya Rosberg.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents