Habari

Kijana aliyejifungia chooni na kusababisha ndege kuchelewa kuondoka kufikishashwa mahakamani Dar

Kijana raia wa Oman, Ally Thabit Ally, anayedaiwa kufanya vurugu kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia na kuichelewesha kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, anaendelea kusota polisi.
img-20160823-wa0019

Ally aliyeichelewesha ndege kwa saa kadhaa anashikiliwa na polisi kabla ya kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uharibifu wa mali, kwa mujibu wa Kamanda Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno.

Wiki iliyopita kijana huyo alifanya vurugu kwa kujifungia chooni na kusababisha kuchelewa kuondoka ndege hiyo iliyokuwa inaanza safari kuelekea Addis Ababa Ethiopia.

Wahudumu walishtukia abiria huyo hakuwepo kwenye kiti kwa muda mrefu na alipogongewa kwenye mlango wa chooni aligoma kufungua akikaa humo kwa zaidi ya dakika 15.

Kutokana na hali hiyo ilimlazimu rubani kuahirisha safari na kuirudisha maeghesho huku watu wa usalama wakifanya jitihada za kumtoa chooni na baada ya kutolewa hakuendelea na safari akawa anachunguzwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Otieno alieleza kuwa wanasubiri kupatiwa taarifa ya thamani halisi ya mali zilizoharibiwa ili afikishwe mahakamani.

Kamanda Otieno alieleza kuwa walibaini abiria huyo ni mwanafunzi wa chuo huko Oman na kwamba katika uchunguzi wao hajatoa sababu za msingi zilizomsababishia kufanya vurugu.

Source: Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents