Burudani

Muigizaji wa filamu ya ‘The Sound of Music’ ya 1965 afariki dunia

Muigizaji mkongwe wa Marekani, Charmian Carr aliyeigiza filamu ya ‘The Sound of Music’ amefariki dunia akiwa na miaka 73 huko mjini Los Angeles.

_91293577_charmian

Chanzo cha kifo cha muigizaji huyo kinadaiwa ni kutokana na kusumbuliwa kwa ugonjwa wa dementia.

Charmian Carr aliigiza kama mkubwa wa familia ya von Trapp Liesl kwenye filamu hiyo ya The Sound of Music ambayo iliyoigizwa mwaka 1965 na kufanikiwa kuipiku filamu ya ‘Gone with the Wind’ ambayo ilikuwa inaongoza kwa wakati huo.

0918-charmain-carr-getty-with-swipe-8
Picha ya Charmian Carr akiwa kwenye filamu ya The Sound of Music

Filamu nyingine alizowahi kuigiza Charmian Carr ni pamoja na Evening Primrose. Lakini pia amewahi kuandika vitabu viwili ambavyo vilivyowahi kufanya vizuri ikiwemo Forever Liesl na Letters to Liesl. Hata hivyo baada ya muda Charmian Carr aliachana na kazi ya uigizaji na aliamua kuingia kwenye kazi ya upambaji.

Tazama hapo chini kipande cha video cha Charmian Carr akiimba wimbo wa Sixteen Going On Seventeen kwenye filamu ya The Sound of Music mwaka 1965.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents