Burudani

Nikki wa Pili aguswa na bomoabomoa Dar, ‘maendeleo kwa ajili ya nani?’

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nikki wa Pili ameguswa na bomoabomoa inayoendelea jijini Dar es salaam kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro kwa kusema tunahitaji maendeleo lakini utu lazima uzingatiwe kwani wanaobomolewa ni watu masikini na maendeleo ni kwa ajili yao.

Nikki wa Pili

Nikki wa Pili amesema watu wengi wanaoishi maeneo yaliyokumbwa na bomoabomoa ni watu masikini na wamehangaika kujenga nyumba hizo ambazo zinabomolewa kupisha upanuzi wa barabara je, hayo maendeleo yanayofanywa ni kwa ajili ya nani?

Unaposikia bomoa mara nyingi huwa makazi yà watu wa chini wajuu wakiguswa ni wachache…….basi hayo maeneo yataendelezwa na kuwa ya wakazi wa hali ya juu au maghorofa ya kumilikiwa na wageni au vyovoyote vile……..lakini wale waliokuwa pale mwanzoni hawataweza kuishi pale….watakuwa pembezoni huko au watabaki bila makazi kabisa…je ni maendeleo kwa ajili ya nani? Je maendeleo ni kufukuza tabaka flani la wengi pembezoni kwakuwa hawana kitu”,amehoji Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Instagam huku akisisitiza kuwa maendeleo yoyote lazima yawalenge watu hao masikini na sio kuwafukuza.

SOMA ZAIDI-Bomoa bomoa Kimara: TANESCO waigomea Tanroards kukata umeme

“kipimo cha maendeleo ni watu haswa watu wa chini walio wengi mkakati wowote wa maendeleo lazima uwalenge hawa…..na msukumo wa mipango miji utokane na wao na historia yao na uhalisia wao sio utokane na vipimo vya kimataifa au misukomo toka wafadhili wa nje”,ameandika Nikki wa Pili .

Bomoabomoa jijini Dar es salaam imeathiri kuanzia maeneo ya Kimara hadi Kibamba ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents