Burudani

Nikki Wa Pili amjibu Lord Eyez kuhusu tuhuma za ‘ubinafsi’

Msanii wa Kundi la Weusi, Nikki Wa Pili ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo, amekanusha taarifa aliyoitoa aliyekuwa member wa kundi hilo, Lord Eyez, kuwa kampuni ya Weusi ina watu wabinafsi.

Rapa huyo amedai sio kweli kwamba wana ubinafsi kama Lord Eyez anavyodai huku akisema laiti wangekuwa wabinafsi basi wasingeweza kuwa na urafiki baina yao.

“Bonta na Joh Makini urafiki wao unazaidi ya miaka 15, mimi na G Nako tuna urafiki zaidi ya miaka 12 ‘so’ watu wenye ubinafsi hawawezi kuwa marafiki kwa ‘fact’ hiyo ndogo unaweza ukapima,” Nikki alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Pia rapa huyo alibainisha baadhi ya mambo kwa kusema kampuni hiyo haina ugomvi na Lord Eyez na muda wowote akikamilisha masharti alioambiwa anaweza kukaribishwa tena upya kufanya kazi na kundi hilo la Weusi kutoka Arusha.

“Lord Eyez na kampuni wapo vizuri na ninafikiri kampuni ilishampa A, B,C zake, na yeye mwenyewe tu akizikamilisha tu hakuna tatizo”. alisisitizia Nikki wa Pili

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents