Michezo

Liverpool wailaza mapema Watford kwa 1-0

Ligi kuu ya soka nchini Uingereza imeendelea hapo jana usiku, huku wapenzi wa soka wakishuhudia mchezo mmoja kuchezwa katika ligi hiyo pendwa zaidi duniani. Majogoo wa London, klabu ya Liverpool wakiwa ugenini, wameweza kuchomoza na ushindi mwembamba wa goli 1 kwa 0 dhidi ya Watford.

Katika mchezo huo uliokuwa mzuri na wa aina yake, mashabiki wa klabu hiyo ya Liverpool wameweza kushuhudia klabu yao ikichomoza na ushindi mwembamba kabisa katika dakika 45.

Shujaa wa mchezo huo, akiwa ni kijana Emre Cam, aliweza kuipatia goli klabu yake, lililoipaisha hadi alama 69 na kukifanya kikosi hiko kuwa karibu zaidi na vinara wa ligi, Chelsea pamoja na klabu ya Tottenham, ikiwa ni msimamo ambao unaonyesha nafasi ya nne kushikiliwa na Manchester city ilhali nafasi ya Tano ikisalia kwa mashetani wekundu Manchester United.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents