Burudani

Nikki wa Pili kumsifia mwanamke wa kichaga katika wimbo wake mpya ‘Sweet Mangi’

Msanii wa muziki kutoka Kundi la Weusi, Nikki wa Pili anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Sweet Mangi’ ambao utakuwa unawasifia wanawake wakichaga.
nikki wa pili

Rapa huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa, wimbo huo amemshirikisha Chidi Benz.

“Wengi wanasema wasichana wa Kichaga hawajui kupenda wanawaza fedha, lakini ukisikiliza wimbo wangu utajua namna wanavyopenda kuliko wanavyofikiriwa na wengi,” alisema Nikki.

Nikki wa Pili amesema wimbo huo utawafanya wanawake wa kichanga kujiamini na kupuuza yale ambayo yanasemwa na watu wa nje.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents