Burudani

Nilikuwa tayari kuwa mke wa pili kwa Diamond kama angemuoa Zari – Hamisa

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kwa kudai kwamba yeye kwa Diamond alikuwa tayari kuwa mke wa pili kama muimbaji huyo angemuoa Zari The Boss Lady.

Wawili hao kwa sasa ameachana na wamekuwa wakitupiana maneno mtandaoni baada Diamond kuanza kuzungumzia madai ya kwamba familia yake inarogwa na mrembo huo.

Akiwa nchini Kenya Mobetto amefunguka kwa kudai kwamba wakati anaanza mahusiano na Diamond alijua ana mwanamke mwingine aitwaye, Zari.

“Wakati nakutana na Diamond nilijua kuna Zari na nilimuuliza, akasema mimi ni muislam na uwezo wa kuoa hata wanawake wawili,” alisema Mobetto. “Na mimi nipoo tayari hata kama ningekuwa nimeolewa halafu mume wangu anataka kuoa mke wa pili ningemruhusu,”

Mrembo huyo alifanikiwa kuzaa mtoto mmoja na Diamond huku Zari naye akimzalia muimbaji huyo watoto wawili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents