Burudani

Video: Waganga hapana lakini nimetumia sana mitishamba – Wema Sepetu

Leo ni siku ya kuzaliwa ya malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ambapo ameandaa tukio maalum kwaajili yake litakalofanyika Ijumaa hii pale Mlimani City. Tukio hilo litaambatana na uzinduzi wa filamu yake aliyofanya na Van Vicker kutoka Ghana ambaye yupo tayari nchini Tanzania.

Katika kuifanya siku hiyo kuwa nzuri, Wema amefanya interview na vituo mbalimbali vya habari ambapo siku ya jana kupitia ThePlaylist ya Times FM alifunguka kuzungumzia kama aliwahi kwenda kwa mganga katika maisha yake.

“Hapana sijawai kwenda lakini nimekuwa nikinywa sana mitishamba kwaajili ya tatizo langu la kukosa mtoto, nimekunywa sana mpaka wanahisi zimeniongezea tatizo,” alisema Wema Sepetu.

Mrembo huyo amedai tataizo la kutopata mtoto ndio kitu ambacho kimekuwa kikimsumbua kwa muda mrefu huku akidai baadhi ya wabaya wake wamekuwa wakitumia hiyo kama njia ya kumuumiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents