Burudani

Nimefikia hatua sitaki tena kuwa mwembamba – Lady Jaydee (+video)

Msanii wa muziki Bongo, Lady Jaydee amefunguka mipango yake kuongeza uzito kwani hataki tena kuwa mwembamba.

Muimbaji huyo amesema kwa sasa yupo kwenye harakati za kuongeza uzito kwa kuhakikisha anakula vizuri ili kufikia lengo lake.

“Ninachoangalia sio nimepate kilo ngapi, sitaki kuwa mwembamba nataka niwe na mwili ambao utaniridhisha, yaani sipendi hivi nilivyo kwa sasa, sipendi kuwa mwembamba tena naona kama mimi sio mtoto mdogo wa kuwa mwembamba sana kiivyo.” amesema.

“Kila mtu anavyofikiria, wengine wanaona wapo sawa lakini mimi nimefikia hatua sitaki tena kuwa mwembamba,” ameongeza.

January 20 mwaka huu Lady Jaydee kupitia Instagram yake aliandika; “Niko kwenye jitihada za ku-gain weight ndani ya siku 10, nimekonda sana hadi najihisi kama mwanafunzi wa Secondary.  Na hii ni kutokana na kazi za kukimbia na kusafiri kila siku na kukosa usingizi wa kutosha mwezi wote wa December na January mwanzoni Kwa umri wangu nahitaji nyama nyama kidogo sio sana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents