Michezo

Nimepania sana kwenda Tanzania – Wayne Rooney

Baada ya kutangazwa rasmi kujiunga na timu yake ya utotoni ya Everton akitokea Manchester United, Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kuzungumzia safari ya Everton nchini Tanzania kwa kusema amepania sana kuja nchini.

Kupitia Mtandao wa Klabu ya  Everton mapema leo akiwa mazoezini, Rooney amesema hajawahi kufika Tanzania kwa hiyo safari ya Klabu ya Everton kwake itakuwa ni fursa nzuri ya kuifahamu Tanzania ikiwa ni pamoja na kujuana na kutambuana vizuri na wachezaji wenzake.

Sijawahi kufika Tanzania, na safari hii nimeipania sana kwani itakuwa ni muda mzuri wa kujuana na wachezaji wenzangu, najaribu kuwaza jinsi mechi za ugenini zinavyokuwa na hamasa hususani kwa mashabiki“,amesema Wayne Rooney .

Wayne Rooney ambaye tayari ameshakutana na wachezaji wengine wa Everton kama Michael Keane,  Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley wakiwa kwenye Timu ya Taifa ya England hakuna shaka yoyote kuwa atakuja Tanzania na kikosi chote cha Everton alhamisi hii ya Tar 13 Julai.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents