Habari

NMB yadhamini Mil.25 kwa ajili ya Michuano ya Golf- Lugalo

Benki ya NMB imetoa udhamini wa Sh. Mil. 25 kwa Mashindano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi Tanzania (NMB CDF Trophy 2022), kama muendelezo wa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Septemba 1, lakini kutokana na sababu mbalimbali mwaka huu yamelazimika kusogezwa kwa mwezi mmoja.

Akizungumza wakati akipokea mfano wa hundi Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwa mdhamini wa muda mrefu na kufanyia maboresho zaidi kwa mwaka huu huku akiweka wazi kuwa timu mbalimbali zimethibitisha kushiriki michuano hiyo, ambayo itahusisha kategori za Watoto (junior), Madaraja (division) ya A, B, na C, pamoja na wanawake na Seniors.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Wateja Maluum wa Benki ya NMB, Getrude Mallya, alisema benki yake imedhamini mashindano hayo kwa Sh. Milioni 25 huku aliwaalika viongozi wa klabu ya gofu Lugalo mbio za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zitakazofanyika Oktoba 1 viwanja vya Leaders Club kwa lengo la kukusanya Sh. Mil. 600 za kusaidia matibabu ya kina mama wenye matatizo ya Fistula nchini.

Mashindano ya Gofu yatafanyika Oktoba 1 hadi 2 mwaka huu kwenye Viwanja vya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button