Habari

Ofisi ya IGP kumuunga mkono Waziri Mkuu Majaliwa

Jeshi la polisi nchini limesema mwezi ujao litahamishia makao makuu yake mjini Dodoma, kuitikia agizo lililo tolewa na Rais Dkt John Magufuli.

pic+igp+vs+seif

IGP Mangu

“Agosti tunahania Dodoma, utafanya hivyo kabla ya waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu”, alisema Nsato Marijani, Kamishna wa oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo alipozugumza na mwandishi wa gazeti la Mwananchi.

Mipango ya wizara na taasisi za umma kuhamia Dodoma , zinatokana na tamko la Rais Magufuli kuwa serikali yake kutaka kutekeleza ndoto ya siku nyingi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhamia katika mji huo uliopo katikati ya nchi.

Siku chache zilizopita Waziri mkuu Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia Dodoma ifikapo Septemba na aliwataka mawaziri wote kumfuata.

Kamishna Marijani alieleza jinsi mpango huo utakavyotekelezwa kwamba mkuu wa jeshi na makamishna kadhaa watatakiwa kuhamia Dodoma, huku baadhi wakibaki na kuendelea na majukumu yao mengine kutokea jijini hapa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents