Burudani

Papa Misifa afunguka haya kuhusu kufukuzwa Kaburu Record

Baada ya hivi karibuni uongozi wa Kaburu Record kutangaza kumfuta umeneja, Msafiri Misifa ‘Papaa Misifa’ kwa kile alichodaiwa alishindwa kufikia malengo ya kampuni hiyo kama walivyokuwa wamekubaliana, meneja huyo wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko azungumzia sakata hilo.
Kassim-Mganga-na-mdau-wa-muziki
Papa Misifa (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Kassim Mganga

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Papaa Misifa amefunguka kwa kusema yeye hajafukuzwa kama uongozi wa label hiyo ilivyoripoti.

“Mimi sijafukuzwa kwanza na sina mkataba na mtu yeyote, wao walikuja kuniomba mimi kama Aljazira ili twende nikamsaidie kuipeleka kampuni yake mbele na tulikubaliana makubaliano. Lakini kumbe yule jamaa alikuwa hajajipanga, kipato hana, tarehe moja mwezi wa saba eti anakwambia mbona hakuna pesa, mbona pesa hazipatikani?,” alisema Papa Misifa.

“Sasa unapataje pesa bila matangazo yoyote, bila kazi alafu unasema unataka upate pesa kwa haraka kwa sababu umewekeza pesa. Kwa hiyo nikagundua nilikuwa nafanya biashara na mtu ambaye hajui biashara, kwa sababu mtu hata ukiwa unauza nyanya ndani ya mwezi mmoja huwezi ona mafanikio hayo ambayo anayazungumzia bila hata kufanya matangazo yoyote. Kwa hiyo mimi pale nimeondoka nimerudi Aljazira, naendelea kusaidia vijana mbalimbali,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents