Habari

Ofisi za CUF Zanzibar zapakwa rangi ya ACT Wazalendo, kisa Maalim Seif

Baada ya tamko la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif kujiunga na chama cha ACT wazalendo, tayari baadhi ya ofisi za CUF Wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba zimeanza kupakwa rangi ya ACT Wazalendo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Chama cha Wananchi CUF Wilayani humo, Saleh Nassor Juma amesema wamepokea maagizo kutoka ngazi za juu za Chama hicho toka jana, kabla ya Maalimu Seif kujiunga ACT Wazalendo.

Maagizo hayo, yamewataka waanze kubadili rangi hizo kwenye matawi yote ya chama hicho.

Uamuzi huo umeanza kutekelezwa mapema leo katika ofisi moja ya Chakechake, ambapo imeelezwa kuwa zoezi hilo huenda likaanza kutekelezwa kwenye ofisi za CUF mjini Unguja.

Tamko la Maalimu Seif kuhamia ACT Wazalendo limepelekea baadhi ya wafuasi wake kuihama CUF akiwemo, aliyekuwa Kaimu mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa Chama Cha Wananchi- CUF  Ismail Jussa Ladhu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents