Burudani

Otile Brown amemsaini msanii mpya chini yake lebo yake

Msanii Otile Brown wa nchini Kenya, amutambulisha msanii mpya chini ya himaya yake ya lebo ya “Just in love”.

Kupitia account yake ya instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 1.5, alimtambulisha Lixsil na kwasasa anaendelea na media tour nchini Kenya muendelezo wa kumutambulisha na kuwarai mashabiki wake wazidi kumfatilia na kumuonesha upendo jinsi wanavyomufanyia yeye.

Ikumbukwe Otile awali mwanzoni mwa mwaka huu wa 2020, aligonga vichwa vya habari baada ya kutangaza kumusaini msanii nyota wakike nchini Kenya Jovial. Lakini hatimae baada ya mda mfupi msanii Jovial alitangaza kujiotoa kwenye lebo hiyo ya ” Just in Love” nakumuacha Otile Brown akijikuna kichwa. Otile Brown anaongoza kwenye orodha ya mastaamastaa wa Kenya wenye video zinazo tazamwa zaidi kwenye YouTube kulingana na takwimu za hivi karibuni kwa mjibu wa taarifa kutoka kampuni ya YouTube, huku majuma mawili yaliyopita Otile Brown alishangilia kibao chake Dusuma kutazamwa mara zaidi ya milioni 10 ndani ya siku 90.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents