Michezo

Ousmane Dembele apewa saa 48 Barcelona

Ousmane Dembele amepewa saa 48 na Barcelona kuamua hatima yake ya kusalia ama kuuzwa baada ya klabu hiyo kumuwekea mezani mkataba mpya wakati kandarasi yake ya sasa na vigogo hao wa LaLiga ikitarajiwa kufikia mwisho mwishoni mwa msimu huu.

Ousmane Dembele has 48 hours to decide on his Barcelona future after new contract offer - Barca could lose Dembele for free as he is out of contract at the end of the season

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24, amebakiwa na muda mchache wa kuamua baada ya Bercelona kumpa ofa mpya kwa wiki kadhaa bila majibu yoyote kutoka kwa nyota huyo, huku miamba hiyo ya soka Hispania ikihofia asije kuondoka bure mwishoni mwa msimu baada ya kandarasi yake kumalizika.

Mshambuliaji huyo wazamani wa Borussia Dortmund anahitaji kusalia Nou Camp, lakini anasisitiza juu ya vile vilivyopuguzwa kwenye dili lake na Barca.

Inadaiwa Dembele anahitaji kiwango kikubwa cha mshahara cha paundi milioni 66.9 kiasi ambacho mpaka kocha wa timu hiyo, Xavi Hernandez akikosa cha kusema na kubaki akimlaumu wakala wa kinda huyo, Moussa Sissoko.

Dembele amejiunga na Barcelona mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmundkwa dau la paundi milioni 96.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents