BurudaniHabari

P Diddy amuunga mkono Kanye West kuvaa T-shirt ya ‘White lives matter’

Rapa huyo mwenye umri wa miaka, 52, alitoa maoni yake kuhusu Rapa mwenzake Kanye West kuvaa T-shirt zilizoandikwa White Lives Matter   wakati wa onyesho lake la Kanye West la nguo la  Yeezy wakati wa Wiki ya Mitindo ya Paris.

Katika mahojiano mapya kwenye “The Breakfast Club P Diddy alisema kuwa.

“Kanye my boy alirudia mara kadhaa akisema Kanye my boy is a super, super, super free thinker,” Diddy alisema. “Na mara nyingi, anachomaanisha ni kama, kueleweka vibaya, unajua ninachosema?, ni ngumu sana kuelewa anachomaanisha Kanye West na mara nyingi watu humuelewa vibaya

Diddy alitoa maoni yake kuhusu onesho la mavazi la Kanye West la Yeezy Season 9, ambalo lilikuwa na T-shirts za “White Lives Matter”.
Diddy aliongeza kuwa “sio lazima wamhukumu Kanye”

“Ninaelewa maisha ya wazungu ni muhimu, lakini sivyo,” Diddy alisema.

“[‘Maisha ya Weusi’] Black lives Matter ilikuwa slogan yetu (kauli mbiu). Hiyo haikuwa kauli mbiu yetu ya kwenda kushiriki na mtu mwingine yeyote … Kwa sababu sasa hivi, sisi ndio tunakufa, tumefungwa, na tumeachwa katika umaskini.”
Mashati ya “White Lives Matter” yalikasirisha wengi katika watazamaji (na zaidi).

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents