BurudaniVideos

Patoranking atueleza alivyokuwa akiuza sumu ya panya kabla ya kutoka (Video)

Watu wengi waliofanikiwa wana historia za kuvutia zilizotawaliwa na maisha magumu hadi kufika kwenye hatua ambayo kila mtu anatamani kuwa kama wao.

Pato1

Msanii Nigeria, Patrick Nnaemeka Okorie ama kama anavyojulikana zaidi kama, Patoranking, ni mmoja wa watu hao.

Akiongea Jumanne hii jijini Dar es Salaam na Bongo5, alidai kuwa miaka ya nyuma alikuwa akiuza sumu ya panya kwenye mitaa ya Lagos.

“Watu wengi hawajui kuhusu Patoranking na kulikuwa na vitu ambavyo ilinibidi nifanye. Nakumbuka nilikuwa nauza sumu ya panya kwenye mitaa ya Lagos lakini hiyo ilikuwa miaka ya nyuma sana. Lakini sasa kila kitu kimebadilika namshukuru Mungu kwa kila kitu,” alisema.

Alidai kuwa hata jina la album yake, God Over Everything limekuja kutokana na jinsi safari yake ya maisha ilivyokuwa na jinsi Mungu alivyombariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents