Bizzare

Penzi la mama na mwana lazua utata Marekani

Mwanamke wa Uingereza na mwanae wa kiume waliopo kwenye uhusiano wa kimapenzi, wamelazimika kujificha baada ya polisi kuwaonya kuwa wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela.

32F7365500000578-3529572-image-a-1_1460106661411

Kim West, 51, na mwanae, Ben Ford, 32, wanaoishi Michigan, Marekani, walidai kuwa wanapanga kufunga ndoa na kuzaa watoto. The Mirror limedai kuwa wawili hao wamejificha baada ya mamlaka kutambua uhusiano wao.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano tangu mwaka 2014 na wanadai wamekuwa wakipeana mapenzi matamu. Kwa mujibu wa sheria za jimbo la Michigan, wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela. West, aliyekulia Islington, London, alipata mimba wakati akisoma California na baada ya kumzaa mwanae akiwa na miaka 19 alimwacha aasiliwe na watu wengine.

December 2013, alipokea barua kutoka kwa mwanae aliyekuwa anawatafuta wazazi wake wa kumzaa. Na tangu wakutane January 2014, walijikuta wakipendana.

Na sasa uhusiano wao una miaka miwili na wanaishi pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents