Burudani

Peter Msechu azungumzia nini anapenda mwanae aje kufanya akiwa mkubwa

Peter Msechu amesema hapendi mwanae Lauren a.k.a Lolo aje kuwa mwanamuziki, bali anataka kumjengea msingi utakaomfanya aweze kusoma na kupata kazi itakayomuingiza kipato cha kudumu.

1378199_355534831249383_901084370_n

“Kama mzazi, mwanangu namlea katika misingi bora anakula, analala mahala pazuri, na hakikisha baadaye anakuja kujitegemea yeye mwenyewe, sitaki ile anakuja kusoma sana halafu halafu baadae afanye muziki hapana,” Msechu alikiambia jana kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Radio, Mbeya.

Kwa hatua nyingine Msechu alisema video ya wimbo wake Fire imechelewa kutoka kwakuwa kuna marekebisho yanafanyika.

“Video ya ngoma ya Fire tuitegemee soon itakuwa inatoka, hivyo kuna marekebisho madogo ilikuwa itoke mapema. Nadhani itakuwa kwenye position ya kutoka ndani ya wiki mbili zijazo kwa sababu kasoro zote tumeshaziweka sawa.”

Msikilize hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents