Bongo MovieBurudani

Proin Promotions waanzisha shindano la vipaji vya uigizaji, mshindi atazawadiwa shilingi milioni 50

Kampuni ya usambazaji wa filamu nchini, Proin Promotions jana imetangaza kuzindua shindano la kusaka vipaji vya uigizaji nchini.

AMVCA-Trophy-
Meneja wa Masoko wa Proin Promotions (katikati) akiongea na waandishi wa habari. Kushoto ni Meneja wa mradi wa kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania(TMT) Joshua Moshi na kulia ni muigizaji wa filamu, Single Mtambalike aka Richie atakayekuwa jaji wa shindano hilo

Shindano hilo lilipewa jina Tanzania Movie Talents lina lengo la kusaka na kukuza vipaji vya wasanii wachanga na litaanza April 1 kwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na Singida.

Mshindi kwenye msako huo atazawadiwa shilingi milioni 50.

Chanzo: BongoMovies.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents