Habari

Picha za kwanza za mgahawa mkubwa wa chakula cha haraka duniani – McDonald’s

Mashindano ya olimpiki yatakapoanza mwezi ujao mjini London, Uingereza, mji huo mkuu utashuhudia wanamichezo bora duniani lakini pia utakuwa nyumbani kwa mgahawa mkubwa wa McDonald’s chini jua pembeni tu mwa uwanja yatakapofanyika mashindano hayo.

Mgahawa huo wa aina yake utahudumia hadi wateja 1,200 kwa saa na kuuza chakula kitakachofikia gharama ya paundi million 3 wakati wa mashindano hayo.
Ikiwa na ukubwa kwa square futi 3,000, jengo la mgahawa huo lililopo jirani na uwanja wa olimpiki,ni kubwa zaidi ya jengo la mgahawa wa kampuni hiyo lililokuwa kubwa zaidi la mjini Moscow, Urusi.

Hata hivyo mgahawa huo wa Urusi utachukua tena sifa hiyo September 9 pale tawi hilo la London litakapobomolewa lote baada ya kumalizika kwa mashindano ya olimpiki kwa walemavu,Paralympics.

Jana, (June 25) McDonald’s iliwaonesha waandishi wa habari muonekano wa mgahawa huo wenye siti 1,500
McDonalds imekuwa wadhamini wa Olimpiki tangu mwaka 1968 baada ya kampuni hiyo kusafirisha kwa ndege vitafunwa aina ya ‘hamburgers’ kwa wanamichezo wa Marekani hadi mjini Grenoble, Ufaransa baada ya kuripotiwa kuwa walikuwa wakimiss chakula cha McDonald’s.

Hata hivyo kampuni hiyo imekuwa ikikosolewa kwa kupigia debe matumizi ya chakula cha haraka katika muda ambao watu wanatakiwa kusherehekea kujihusisha na mazoezi kama njia bora ya kuishi kwa afya.
Mgahawa huo maalum wa London utaanza kuhudumia wateja wake kesho kutwa (June 28) siku moja baada ya sherehe za ufunguzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents