Habari

Collo (Kenya) kumtungia wimbo mtoto wake

Tumeshuhudia wasanii kadhaa miezi ya hivi karibuni wakiimba nyimbo kwaajili ya watoto wao. Baada ya Beyonce kijifungua mtoto wa kike, Jay-Z ambaye ni baba wa mtoto huyo Blue Ivy aliandika wimbo uitwao Glory.
Muda mfupi baadaye Nas akaandika wimbo kwaajili ya mwanae wa kike Destiny uitwao Daughters. Kwa Tanzania wasanii kama Bob Ludala na Banana Zorro nao walishawahi kuwatungua nyimbo watoto wao.
Mwanadada wa Kenya Wahu naye alishawahi kumwimbia mwanae wa kike Tumiso kwenye ‘Sweet Love’.
Mzazi mpya mwenye kujivunia status hiyo ni rapper wa zamani wa kundi la Kleptomaniac la Kenya aliyejipa jina la King wa Rap, Collo.
Amerekodi wimbo maalum kwa binti yake aitwaye Tawala. Katika wimbo huo uitwao Dreamer Collo ameishirikisha bendi ya Sauti Sol.

“Ni kama mwaka mmoja tangu Mungu anijaalie mtoto wangu Tawala. Nimejisikia tu kuwa nahitaji kufanya kitu special kwa malkia wangu,” Collo aliliambia gazeti la The Star Kenya.
Awali Collo alidai kuwa anataka kumfundisha mwanae muziki. Katika mahojiano ya awali na gazeti hilo, Collo alidai kuwa tayari amepanga kumpeleka mwanae akajifunze kupiga piano na violin.
Binti yake Tawala Oyieli Majale alizaliwa July mwaka jana, mama yake akiwa mpenzi wake wa siku nyingi, Phoebe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents