Habari

“Prof. Lipumba na wafuasi wake ni watu wanaoamini ushirikina”

Pande mbili za Viongozi wa Chama cha Wananchi  (CUF) wameanza kutupiana lawama na kushikana uchawi, baada ya mvutano uliopo kati ya upande wa Maalim Seif na Prof. Ibrahim Lipumba kuendelea kuota mizizi.

Tokeo la picha la CUF

Upande wa CUF unaomuunga mkono Maalim Seif  kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Mbarala Maharagande amedai kuwa Maalim Seif analindwa na haki na si ushirikina kama ilivyo kwa Mwenyekiti wa (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba.

“Lipumba na wafuasi wake ni watu wanaoamini sana mambo ya ushirikina katika kufanikiwa mipango yao michafu dhidi ya Taasisi ya CUF. Mara kadhaa wameonekana kutumwa wafuasi wake kwenda kununua Mbuzi kwa ajili ya kazi hiyo katika mnada wa Vingunguti. Kamati ya ushirikina inaongozwa na Abdul Kambaya na Hamisi Hassan kwa upande wa Tanzania Bara na Mohamed Thiney na Nassor Seif kwa upande wa Zanzibar”ameandika Maharagande kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwa upande mwingine, Maharagande amesema Profesa Lipumba na kundi lake wameshindwa kuigawa CUF kama ambavyo walikuwa wakitegemea na kudai uchaguzi mdogo wa udiwani umeweza kutoa majibu kwani wagombea wote wa Lipumba wamepata kura chache sana na kuonekana wazi kuwa watu hao hawakubaliki katika jamii.

“Lipumba na wafuasi wake wameshindwa kuigawa CUF na mbeleko ya CCM inakaribia kukatika kutokana na kutoona faida yao hasa katika ushindani wakati wa uchaguzi. Watazania washawafahamu kuwa ni vibaraka, wasaliti na wachumia tumbo, hawapo kwa dhati ya kutaka Mabadiliko ya kweli kisiasa kutokea hapa nchini. Mgombea wa Lipumba katika Kata ya Reli, Mtwara Mikindani kushika nafasi ya nne kwa kupata kura 21 baada ya CCM, CHADEMA, na ACT katika Jimbo linaloongozwa na Mbunge kutoka ‘CUF MAKINIKIA’ ni salamu tosha kwa Maftaha Nachuma na Lipumba kuwa hawakubaliki na hawana mchango wa maana kwa CCM” ameandika Maharagande.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents