Burudani

Professor Jay alivyomuingiza P The Mc katika muziki

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, P The Mc amesema ushawishi alionao Professor Jay katika muziki umechochea hata wazazi wake kumruhusu kufanya muziki.

Rapper huyo wa kundi la SSK katika mahojiano na Bongo5 amesema kazi za Professor Jay toka mwanzo mtu yeyote anaweza kuzisikiliza na ndio chanzo cha kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwa vijana wengi kuingia katika muziki wa rap.

P The Mc amesema kabla ya Prof Jay muziki wa hip hop Bongo ulikuwa unaoneka ni muziki fulani wa vijana tena hasa wale wa masikani ambao hawana shughuli yoyote ya kufanya lakini aliweza kubadili mtazamo huo.

“Ila Professor Jay aliweza kuwashawishi watu kwa ule muziki ambao unaweza kusikilizwa na Rais, Mbunge na Mawaziri, maana yake ni kwamba wazazi wangu walishawishika kusikiliza muziki wa Professor Jay”amesema P The Mc.

“Nikitaka kufanya muziki wataniambia unatakiwa ufanye kama huyu kwa sababu anachokifanya ni kizuri, so ni lazima niamini amewashawishi wazazi waniruhusu niingie kwenye muziki” ameongeza.

P The Mc kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Mademu Wangu’ ambayo amefanya remix kutoka kwenye ngoma ya Marehemu Ngwea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents