Habari

Professor Jay alivyotua kwenye uzinduzi wa foundation yake, Tsh Mil. 800 zachangishwa

Msanii wa muziki @professorjaytz tayari amefika Mlimani City jijini Dar Es Salaam kwaajili ya uzinduzi wa foundation ya kusaidia wagonjwa wa figo ambapo jumla Mil. 800 zimekusanywa.

Msanii wa muziki na Mkurugenzi wa Kings Music @officialalikiba amekuwa ni mmoja kati ya wasanii wachache wa muziki waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya @professorjaytz foundation kwaajili ya kusaidia wagonjwa wa figo.

Licha ya kufanya show maalum kwa ajili ya Professor na kuchangisha pesa akiwa ukumbini hapo kutoka kwa wageni, yeye pamoja Kings Music wametoa Tsh Mil. 5 kwaajili ya mchango wa taasisi hiyo.

Wasanii wengine ambao waliahidi ni muimbaji @jidejaydee ambaye aliahidi Tsh Mil. 5.

Rapa Joh Makini na yeye hakuwa nyuma kwani kwa kushirikiana na Weusi walitoa Tsh Mil. 1.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents