Burudani

Quick Rocka akanusha kuwa na uhusiano na Kajala

Bishoo, Quick Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu, Kajala Masanja.

Quick-Rocka

Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Quick amesema ana girlfriend hivyo uvumi huo unaweza ukamharibia uhusiano wake.

“Nasema hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa na Lamata. Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga chemistry. Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi moja inabidi mchongo tuufanikishe,” alisema rapper huyo.

“I have a girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents