Burudani

JB atoa ushauri kwa waigizaji wa kike, asema wengi hawako ‘serious’

Muigizaji, mtayarishaji na muongozaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB, amesema waigizaji wengi wa filamu wa kike hawako serious.

10684039_1398440703714235_1115333071_n
JB akiwa location kushoot video yake ijayo, Mzee Swagga

JB ambaye kupitia kampuni yake, Jerusalem Films, aliongoza filamu aliyoigiza Shamsa Ford, Chausiku inayotajwa miongoni mwa filamu bora za mwaka huu, amesema waigizaji wa kike wanashindwa kutumia umaarufu wao kufanya filamu bora.

“Majina yao ni makubwa sana lakini useriousness kwenye filamu ni mdogo sana,” JB ameiambia Bongo5.

“Kwa majina yao makubwa, tungeshirikiana nao kwa ukubwa ule na wakawa serious, film industry ingekuwa mbali sana kuliko hapa tulipo. Mimi nawaasa tu, wana kipaji kikubwa, wawe serious na waweke akili yao kwenye kazi hii na watafanikiwa.”

JB aliongeza kuwa wasanii hao wengi wao wanapendwa hivyo kazi yao ni rahisi zaidi kama watajituma na kupenda kazi yao iliyowapa majina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents