Habari

Rais Magufuli afika nyumba kwa Mabeyo kutoa pole baada ya kufiwa na mtoto wake – Picha

Rais Magufuli afika nyumba kwa Mabeyo kutoa pole baada ya kufiwa na mtoto wake - Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

 

 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza sala pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na familia yake wakimuombea marehemu   Nelson Mabeyo ambaye alifariki kwa ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.

Chanzo Michuzi…

PICHA NA IKULU

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents