Habari

Rais Magufuli anafahamu anakoipeleka Tanzania – Mengi

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na mmiliki wa Kampuni ya IPP Limited, Reginald Mengi amewataka Watanzania kuwa na subira kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwani anakoipeleka nchi anakujua mwenyewe huku akiwaomba tuendelee kumuombea.

BAR15
Kutoka kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Reginald Mengi

Reginald Mengi amesema anaamini Rais Magufuli anachokifanya ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu hivyo hatuna budi kumuombea na kumpa muda wa kutosha ili aweze kuipeleka Tanzania mbele.

Naamini Rais Magufuli @MagufuliJP anafahamu anakopeleka Tz kwa manufaa ya Taifa.Tumpongeze,tumuombee.Tumpe nafasi na muda.Tuwe na subira.” ameandika Reginald Mengi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Reginald Mengi ni moja ya matajiri ambao wanaushawishi mkubwa kwa vijana ambao wana ndoto za kuja kuwa wajasiriamali wakubwa nchini hii ni kutokana na Tips anazotoa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu ujasiriamali.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents