Michezo
Jo-Wilfried ayaaga mashindano ya Aegon ya Uingereza
Mcheza tenisi raia wa Ufaransa Jo-Wilfried Tsonga ametupwa nje ya michuano ya Aegon na Gilles Muller katika michuano inayoendelea nchini Uingereza.
Mcheza tenisi raia wa Ufaransa Jo-Wilfried Tsonga
Katika seti ya kwanza Muller alishinda kwa 6-4 na seti ya pili akishinda kwa 6-4 na hivyo kufanikiwa kumtoa kwa jumla ya seti mbili katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo.
Licha mchezaji huyo mkubwa katika medani ya mchezo wa Tenisi kutolewa katika michuano hiyo mikubwa , wengine waliotolewa mapema ni pamoja na Andy Murray, Stan Wawrinka na Milos Raonic.
BY HAMZA FUMO