Habari

Rais Magufuli awafukuza kazi watumishi 9932 wenye vyeti feki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema amewafukuza kazi watumishi 9932 waliobainika wana vyeti feki huku akitaka wasilipwe mishahara yao ya mwezi huu.

Rais Magufuli ameyasema hayo Ijumaa hii wakati akikabidhiwa na Waziri Angella Kairuki orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Alisema Rais Magufuli “Hizo nafasi 9932 zitangazwe ili wasomi hawa waanze kuziomba. Hawa wafanyakazi 9932 leo ni tarehe 28 ninajua wanajijua lakini na majina yao myaandike kwenye magazeti kwasababu ndiyo sera za uwazi, kama ulikuwa na baba yako ni kihio unamjua hapa moja kwa moja.”

“Nataka watu wajifunze wametuibia hela katika kipindi chote walichokuwa wakifanya kazi hawana qualification lakini wamekaa pale kwenye position ambazo hawakustahili kuwepo hapo, hawa ni majambazi na majizi kama yalivyo majizi mengine kwasababu hata pefomance kwenye kazi zao hawakuweza kuperfom vizuri.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents