Habari

Rais Magufuli awaonya TAKUKURU (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 28, 2019 ameipongeza TAKUKURU kwa kufanya kazi nzuri ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini kwa mwaka 2017/18 na kuwataka waongeze makali.

Akiongea kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa ripoti ya TAKUKURU na kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, amewaonya pia TAKUKURU kutowaonea watu katika utendaji wao na kuwataka wafanye kazi kwa bidii.

Katika ripoti hiyo iliyosomwa na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Kamishna Diwani Athuman, imeeleza kuwa “Katika kipindi cha mwaka 2017/18 TAKUKURU imefanikiwa katika utendaji wake wa kazi kwa 81.4% na kuweza kuokoa kiasi cha TSh Bilioni 70.3 katika mwaka huo.”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents