HabariVideos

Rais Samia alivyosaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Kifunda Mbeya baada ya kusimama (+ Video)

Kituo cha Afya cha Kifunda kilianzwa kujengwa mwaka 2017 kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali lakini hakikuweza kumaliza kwa wakati hivyo kuongeza changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya lakini mwaka 2021 Rais Samia Suluhu alitoa fedha kwa ajili ya kuendeleza mradi huo kwa hatua kubwa zaidi.

Wananchi wa kijiji cha Kifunda wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuweza kujenga kituo hicho cha afya ambacho kilichukua takribani miaka 4. “Kituo hichi cha afya cha kifunda kitakapo kamilika kitatusaidia sana sisi wananchi wa kijiji cha kifunda pamoja na vijiji vya jirani ambavyo ni vya kata ya Itete hasa kwa kina mama.

Kwa sisi akina mama itatupunguzia ile adha ya kina mama kujifungulia njiani na kupunguza vifo vyakina mama wanaojifungua na watoto wachanga,” alisema Huruma Kamara mwananchi wa Kifunda.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Busokelo, Christopher Mwasongela amesema kuwa uwe na kituo hicho cha afya utawasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma na pia kupunguza gharama. “Kama mnavyoona huku ni milima na mabonde, mvua inanyesha kila mara na usafiri wenyewe ndio huo barabara zetu bado hazijakaa vizuri lakini kwa kupatikana sasa hivi maeneo haya kituo inawapunguzia adha ya kwenda mbali kwa ajili ya kwenda kupata huduma za afya,” alisema Mwasongela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents