Habari

Rais Samia ateua na kutengua, Msigwa na wengine wapeta

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Septemba 23, 2023 amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:

1. Amemteua, Said Othman Yakubu kuwa Balozi.

Kabla ya uteuzi huu, Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

2. Amemteua, Mohamed Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maofisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

3. Amemteua Dk Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dk Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).

4. Amemteua Dk Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.

5. Amemteua, Hassan Bakari Nyange kuwa
Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo.

Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.

6.Amemteua, Reuben Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.

7.Amemteua, Francis Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki – Kilindi Handeni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents