HabariMichezo

Raja CA waupata ujumbe wa Simba, wajibu mapigo

Wakati joto la mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baina ya Mnyama @simbasctanzania dhidi ya Raja Club Athletic likizidi kushika kasi, huko mitandaoni nako mambo ni moto.

Timu ya Raja Club Athletic inaonekana kama vile umewafikia ujumbe wa Klabu ya Simba wa ”Moto ni Ule ule, Kwa Mkapa hatoki Mtu.” huku ujumbe huo ukionogeshwa na picha la kibabe.

Miamba hiyo ya soka Afrika nayo imeposti ujumbe huo wa Simba ukiambatanishwa na kipande cha video kwenye akaunti yao ya kijamii ya twitter na kuwandika ” Habari marafiki wa Simba SC, Kiswahili changu vipi ?,”

Simba SC na Raja Club Athletic wanatarajia kukutana Benjamin Mkapa mchezo wa Ligi ya Mabinbgwa Afrika Jumamosi ya Februari 18, 2023.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents