Michezo

Ratiba ya ligi kuu Tanzania bara weekend hii

Baada ya kusimama kwa muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.

Michezo ya leo Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam – mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi, zitafanyika saa 10.00 jioni.

Mechi za ligi hiyo ambazo huoneshwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho ni mdhamini mwenza wa VPL, itaendelea Jumapili ambako Kagera Sugar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huo utakuwa saa 10.00 jioni

Mchezo mwingine utazikutanisha timu za African Lyon ya Dar es Salaam dhidi Stand United ya Shinyanga utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huu, utaanza saa 8.00 mchana kwa kuwa kanuni zinaridhia.

Mtibwa Sugar ya Morogoro watakuwa wageni wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo wakati Mwadui FC, kwa upende wake watawaalika JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga huku Majimaji wakiwa ni wenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Source: tff.or.tz

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents