Habari

RC Makonda amkabidhi Kamishna Sianga majina 97 ya wauzaji wa dawa za kulevya, wawili majina yao yaanikwa

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya Rogers Sianga majina 97 ya watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi kamishna wa kupambana na Madawa ya kulevya Rogers Siyanga list ya majina 97 ya watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya.

Aidha watuhumiwa wawili kati ya hao, Chidi Mapenzi (mume wa Shamsa Ford) pamoja na Ayub Mfaume wametakiwa kukamatwa leo.

Akizungumza na waandishi Jumatatu hii mbele ya Kamishna mpya huyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, Makonda amedai katika list hiyo mpya wako watoto wa viongozi wakubwa pamoja na vigogo wengine wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

“Style yangu ni kuwasema hadharani na haya majina 97 ninamkabidhi kamishna siyo kwamba mkoa wa Dar es salaam tunatoka kwenye vita dhidi ya Madawa ya kulevya, sisi ndo moto umekolea, tunamkabidhi yeye ili kupitia vyombo vyake anaweza kushughulika na mtu yeyote aliyoko ndani na nje ya nchi. Na hii list ambayo tumemkabidhi ni ya wafanyabiashara wakubwa, na tutaendelea mpaka kwenye list ya saba, kwa hiyo leo tupo kwenye list ya tatu lakini bado kuna list 4 mbele yetu,” alisema Makonda.

Aliongeza, “Viongozi wa dini tunaomba mtuombee, kwa sababu kwenye kumbukumbu za nyuma mlijatwa kwenye biashara ya Madawa ya kulevya, sitaona aibu kuwashughulikia, Mungu utaratibu wake ni mzuri sana na sisi tutaendelea na mapambano mpaka mwisho, kwa hiyo viongozi wa dini mnatakiwa kujiandaa kuna mambo ya kiuchunguzi yanaendelea. Kwahiyo sisi tumekukabidhi majina ya watu 97 na sisi tumebaki na nakala,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents