BurudaniHabari

RECAP: Baba levo na Harmonize walivyojidhalilisha kugombania hela ya kamari

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la Baba levo kudai kupigwa na Harmonize kwenye Kamari.

@el_mando_tz anasema kauli ya Baba levo ni kwamba ameumizwa na Harmonize ingawa upande wa Harmonize haujatoa kauli yoyote mpaka sasa.

Anasema kuwa Baba levo kuleta ugomvi wao mitandaoni ni kuja kujidhalilisha kwa kugombani hela ya Kamari ambayo wamepewa na mtu ( Sio hela yao)

@el_mando_tz anasema Kamari ni kitu cha kawaida ila ikifikia kwenye ugomvi inakuwa mbaya, tumeona wasanii wengi wakipoteza maisha kwa sababu ya kamari hivyo sio jambo zuri kugombana.

Anaongeza Baba levo kwenda Polisi sio sawa kwani wangeweza kumaliza maana ni ugomvi uliotokana na Kamari na pia amesema Harmonize alikuwa kalewa hivyo hakuwa sawa.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi???

Ukitaka kufuatilia uchambuzi wote tembelea akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Host: @el_mando_tz Cameraman @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents