Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

RECAP: Mapungufu EP mpya ya Rayvanny ‘5 for You’

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameichambua EP mpya ya Rayvanny iliyopewa jina la 5 FOR YOU ambayo ina ngoma 5 na ngoma moja ni kama Bonus.

@el_mando_tz ameichambua kwa pande zote mbili, upande wa mazuri yake na upande wa mapungufu yake hasa kwenye upande wa uandishi na ujume kwa ujumla, kwa upande wa kusema EP ni kali au sio kali amesema kuwa tuipe muda bado mapema.

@el_mando_tz anasema kuwa ukiisikiliza EP ya Rayvanny kuna kitu kimepungua kwenye upande wa Uandishi na hata upande wa melody za Rayvanny.

Kuna nyimbo ukisikiliza kwa mara ya kwanza unamuona Rayvanny kutokana na sound yake.

Anaongeza kuwa kitu kiaya kwenye sanaa ni kwamba kadri msanii anavyoendelea kuwa mkubwa hata uandishi wake unashuka, hiyo huchangiwa na mambo mbalimbali.

Msikilize @el_mando_tz kisha toa maoni yake kwamba unakubaliana naye kwa asilimia ngapi??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents