Burudani

Ridhiwani amzungumzia Rais mstaafu Kikwete kama ana mpango wa kuendelea kuwasaidia wasanii

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema baba yake hawezi tena kufanya harakati za kusupport wasanii kama zamani kwa kuwa tayari umri wake umeenda na anahitaji kupumzika.


Rais mstaafu Kikwete akiwa na msanii wa muziki Niki wa Pili kabla hajastaafu

Akiongea na Bongo5 weekend hii akiwa katika uzinduzi wa video ya Belle 9, Ridhiwani alisema wao kama watoto wa Rais mstaafu wataendelea kuwasaidia wasanii wa muziki pamoja na vijana.

“Unajua kwa sasa hivi yule mbwana mkubwa umri wake umekwenda sana. Lakini Mungu amemjalia ana mwili muzuri,” alisema Ridhiwani. “Unajua kipindi kile yupo Ikulu sisi ndio tuliokuwa tunafanya kazi kubwa ya kumuunganisha na wasanii. Kwa sababu kwake ni vigumu kujua kama kuna mtu anaitwa Belle 9, kujua kuna mtu anaitwa Mwana FA kwa sababu yeye amekulia katika vizazi vya akina Sikinde, kwahiyo muziki wa kizazi kipya tunamuunganisha sisi,”

Aliongeza, “Tumshukuru sana mzee wetu alikuwa mwepesi sana kuwasaidia wasanii katika kuhakikisha wanafika sehemu fulani. Lakini pamoja na hilo sisi ambao tumebaki, tuendelee kufanya yale ambayo mzee wetu alikuwa anafanya kwa kusaidia vijana na kuangalia mambo yanaenda vizuri,”

Mbunge huyo ni mmoja kati ya wadau wa karibu ambao wanamshika Belle 9 katika kuhakikisha anafika sehemu fulani katika muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents