Burudani

Rihanna ataja mataifa nane Afrika atakayozindua bidhaa zake

Mwanamuziki Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna ametangaza kuwa bidhaa zake za urembo za Fenty Beauty na Fenty Skin zitaanza kupatikana katika nchi nane za Afrika kuanzia mwisho wa mwezi huu.

Katika chapisho lake katika mtandao wa kijamii, nyota huyo wa muziki wa pop alisema “amekuwa akiungojea huu wakati” na kwamba huu ni “mwanzo tu”.

Bidhaa hizo za urembo zitapatikana Botswana, Ghana, Kenya, Namibia, Nigeria, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Rihanna, alizindua Fenty Beauty mwaka 2017 kwa ushirikiano na kampuni ya bidhaa za kifahari ya LVMH (Moët Hennessy Louis Vuitton).

Rihanna ana utajiri wa thamani ya $1.7bn (£1.2bn), huku makadirio ya $1.4bn yakitokana na thamani ya Fenty Beauty.

Kampuni hiyo iliripotiwa kutengeneza kiasi cha $100m (£72m) katika siku zake 40 za kwanza.

Kampuni yake imetengeneza pesa nyingi zaidi kuliko bidhaa zingine za urembo zilizoanzishwa na watu mashuhuri kama vile Kylie Jenner’s Kylie Cosmetics, KKW Beauty ya Kim Kardashian na Kampuni ya Honest ya Jessica Alba, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents