Michezo

Rio Ferdinand astaafu kucheza soka, ampa sifa nyingi Sir Alex Ferguson

Rio Ferdinand, 36 aliyekuwa beki Manchester United na timu ya Taifa ya England ametangaza kustaafu soka.

00542A2D00000258-3103651-Ferdinand_poses_with_then_Manchester_United_manager_Sir_Alex_Fer-a-11_1432990672167

Rio ametangaza kustaafu soka baada ya klabu ya Queens Park Rangers kutangaza kumtema kwenye kikosi chake. Alisema hayo katika mahojiano na BT Sport, na aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe Rebecca ambaye wamezaa naye watoto watatu.

na-mkewe
Rio Ferdinand akiwa na marehemu mkewe Rebecca

Ferdinand alimpa sifa kocha wake wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni mfano wa kuigwa kutokana na ujuzi wake.

July 2002 Rio alikuwa beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United kwenda Manchester United kwa pauni milioni 30.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents