Habari

RIPOTI: Kukubalika kwa Rais Magufuli kwaporomoka nchini, CCM inakubalika zaidi kwa wazee na watu wasio na elimu

Leo Julai 05, 2018 Twaweza wamezindua ripoti yao mpya waliyoiita Maoni ya Wananchi kuhusu Ushiriki, Maandamano na Siasa, ambapo imeonesha kuwa kukubalika kwa utendaji wa Rais Magufuli nchini Tanzania kumeporomoka kutoka  asilimia 71 mwaka 2017 hadi asilimia 55.

Takwimu hiyo inaonesha kuwa kuporomoka huko ni kukubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya marais waliokwisha kuiongoza Tanzania kama jedwali hapo juu linavyoonesha.

Kwa upande mwingine pia ripoti hiyo imeonesha kuwa asilimia 76 ya wazee wenye umri kuanzia miaka 50+ wana uwezekano mkubwa wa kusema wapo karibu na CCM kuliko vijana waliochini ya miaka 30 ambao ni asilimia 49 .

CCM pia inakubalika zaidi na Wanawake ambapo asilimia 63 wapo karibu na chama hicho huku wanaume wakiwa ni asilimia 53.

Kundi lingine kubwa la Watanzania ambao wana kikubali zaidi chama cha mapinduzi ni watu wasio na elimu ambao ni asilimia 66, elimu ya msingi 61% huku watu wenye elimu ya sekondari na kuendelea wakiwa ni asilimia 46, kama jedwali linavyoonesha hapa chini.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents