Michezo

Robinho kuozea Jela

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Robinho (40) ameambiwa na majaji nchini Brazil kwamba lazima atumikie kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la ubakaji nchini Italia.

Mwaka 2017, Robinho alihukumiwa nchini Italy kifungo cha miaka tisa jela kwa kitendo cha kushiriki katika kundi la unyanyasaji wa kingono ambalo walifanya kosa hilo mwaka 2013 kwenye Club moja ya usiku alipokuwa akiichezea AC Milan.

Kutokana na changamoto ya Taifa la Brazil sasa imeamua kwamba ni lazima atumikie kifungo cha jela nchini Brazil na tayari majaji wa Mahakama ya Juu ya haki za nchini humo wamepiga kura kuthibitisha hukumu hiyo.

Kwa mujibu wa wakili wake Robinho anataka kesi yake isikilizwe upya nchini Brazil kwa misingi ya uhuru wa kitaifa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents