Burudani

Mwili wa Mohbad bado unachunguzwa

Miezi sita baada ya miti yake kufukuliwa matokeo ya uchunguzi wa maiti ya Mohbad yatakuwa tayari baada ya wiki 4 zijazo.

Dokta Richard Somiari, Mkurugenzi wa kituo cha DNA na uchunguzi katika Jimbo la Lagos, alisema kwamba matokeo ya uchunguzi wa maiti ya Mwimbaji aliyefariki Ilerioluwa Aloba (Mohbad) yatakuwa tayari katika wiki tatu hadi nne zijazo.

Kifo cha Mohbad kilizua utata mkubwa sana na kusababisha Serikali ya Jimbo la Lagos kufanya uchunguzi juu ya kifo hicho.

Uchunguzi huo ulianza mnamo Oktoba 13, 2023, unafanyika katika Mahakama ya Mwanzo ya Ikorodu.

Dokta Somiari alimwambia mchunguzi wa maiti, Hakimu Adedayo Shotobi “Tunatarajia kupata seti ya kwanza ya matokeo ya uchunguzi wa maiti baada ya wiki tatu hadi Nne ili kuthibitisha kifo cha Mohbad”.

“Tuna mahali ambapo vitu vinahifaddhiwa kwa usalama na usalama wa matokeo, kuna utaratibu wa kufuatilia sampuli zilizohamishwa nje ya Nchi” alisema Dokta Somiari.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents