Michezo

Ronaldo amgaragaza Messi kwa mkwanja

Jarida maarufu la Forbes limetoa orodha ya wasanii na wanamichezo walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2017 ambapo mchezaji wa Real Madrid  ndiye aliyeongoza orodha hiyo kwa upande wa wachezaji wa mpira wa miguu akifuatiwa na hasimu wake, Lionel Messi kutoka klabu ya Barcelona.

Tokeo la picha la lionel messi and ronaldo
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo

Ronaldo ameingia kwenye 10 bora ya watu maarufu walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka huu akishika nafasi ya 5 nyuma ya P-Diddy,Jay Z, Beyonce na Drake.

Kwa upande wa wachezaji wa mpira wa miguu Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyeingia kwenye orodha hiyo akiingiza Dola milioni $93 za kimarekani.

Ronaldo ameingiza mkwanja huo kupitia kampuni zake za mavazi, Hotels na matangazo kibao makubwa ya biashara .

Mchezaji mwingine wa mpira wa miguu aliyemfuatia Ronaldo ni hasimu wake Lionel Messi anayekipiga kunako Klabu ya Barcelona yeye ameingiza mkwanja wa kiasi cha Dola milioni $80 za kimarekani akiwa ameshika nafasi ya 14 kwenye orodha ya watu maarufu duniani walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka huu.

Lionel Messi ameingiza mkwanja huo kupitia mkataba wake na Klabu ya Barcelona na Kampuni ya mavazi ya Adidas .

Tazama Orodha kamili HAPA

By Godfrey Mgallah

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents