Rostam aliangukia Kanisa

Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya

Rostam aliangukia Kanisa

 

Mwandishi Wa Habari Leo

Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Amkeni ya Usharika wa Kinondoni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambako alikuwa mgeni rasmi.

Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki na hivyo ni vizuri wakaitumia fursa hiyo kuliombea taifa. “Nawashukuru kwa kunialika kuwa mgeni rasmi leo hii…ni ishara kwamba mmeamua kupuuza vijimaneno na upuuzi wa vijiweni.

Nafurahi kuwa miongoni mwenu….hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,’’ alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo. Alisema inasikitisha kuwa katika zama hizi watu wanachukiana hadi kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo.

“Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,’’ alisema. Mbunge huyo ambaye katika siku za karibuni jina lake limekuwa likitajwa katika mijadala mbalimbali bungeni alisema licha ya matatizo ya kisiasa yanayolikabili taifa sasa, kuna matatizo ya jamii ambayo alisema ni vizuri yakashughulikiwa kama ya ndoa kuvunjika, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, madanguro, kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya na mengine yanayoongeza mmomonyoko wa maadili.

Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini.

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents