HabariMichezo

Sakata la Kocha mpya wa Singida Fountain Gate, Ernst Middendorp kuondoka

Mpaka sasa Klabu ya @singidafountaingate haijatoa taarifa rasmi kuhusu Kocha wake, Ernst Middendorp ambaye amehusishwa kutimka zake wiki mbili tu tangu kusaini Mikataba.

Taarifa zisizo rasmi ni kwamba Kocha, Ernst Middendorp amerudi kwao kutokana na matatizo ya kifamilia

Lakini Mitandaoni kumekuwa na taarifa kuwa Kocha huyo amebwaga ‘MANYANGA’ kutokana na kupangiwa Wachezaji kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Future.

Septemba 2, Singida Fountain Gate mbele ya Waandishi wa Habari walimtangaza, Ernst Middendorp kama Kocha mpya huku wakisema kuwa malengo yao ni pamoja na Kuuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Je, Kocha kaondoka kwa sababu ya kupangiwa Wachezaji, au kaenda kwao kutokana na matatizo ya kifamilia.?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents